Home Soka “Naitaka Nusu Fainali” Benchika Atamba

“Naitaka Nusu Fainali” Benchika Atamba

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Simba sc Abdelhack Benchika ametamba kuwa anataka kikosi hicho kifuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo leo usiku wataivaa Al Ahly Fc katika mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Benchika amesema hayo wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuelekea mchezo huo ambapo ameeleza kuwa anataka kuweka historia kwa kufuzu hatua hiyo na hilo litafanikiwa endapo ataibuka na ushindi katika mchezo wa leo.

“Nataka kuivusha Simba kwenye hatua hii ya robo fainali na kwenda nusu fainali, hayo ni malengo yangu na yetu sisi hadi wachezaji, nataka tuende mbele zaidi tofauti na ambapo Simba huwa inafikia, safari hii nataka kuivusha Simba na najua wachezaji wangu wapo tayari” amesema Kocha Mkuu wa Simba Sc, Abdelhak Benchikha.

banner

Simba sc inapaswa kuhakikisha inapata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano jijini Cairo Misri ambapo huwa ni vigumu kuifunga Al Ahly inapokua katika uwanja wake wa nyumbani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited