Site icon Sports Leo

Namungo Yatelekezwa Angola

Namungo FC imezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Luanda nchini Angola baada ya mamlaka kudai wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virusi vya Corona.

Mpaka wakati wa kuandika taarifa hii timu ipo uwanja wa ndege huku utata ukitawala kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutaka msafara mzima ama urudi Tanzania au uende karantini.

Namungo ipo Angola kuchuana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika mechi ya kombe la shirikisho katika mchezo wa awamu ya kwanza.

Exit mobile version