Beki wa klabu ya Yanga sc Abdala Shaibu Ninja amerejea katika kikosi cha timu hiyo akitokea katika majeraha baada ya kuwa nje kwa takribani wiki tatu akitibu majeraha.
Kurejea kwa beki huyo imekuwa ni faraja kwa kikosi hicho kuelekea katika mchezo mgumu wa ligi kuu dhidi ya watani wao wa jadi Simba sc ambao utafanyika kesho mkoani Dar es salaam katika uwanja wa mkapa.
Kurejea kwa beki kunafanya klabu hiyo iwe na uhakika wa ulinzi akiungana na Bakari Mwamnyeto na Dickson Job huku Lamine Moro akiwa amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.