Kiungo Maestro wa klabu ya Yanga sc Haruna Niyonzima amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga Kariakoo baada ya ule wa awali kuelekea mwishoni.
Kuongeza mkataba kwa kiungo huyo kumetokana na mapendekezo ya kocha Cedrick Kaze kuhitaji kiungo huyo asalie kikosini licha ya kutokua na uhakika wa kuanza mara kwa mara kikosi cha kwanza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Tupo vizuri kwa ajili ya kufanya usajili ambao ni pendekezo la mwalimu, ripoti ipo tayari na tutaitumia katika kuboresha kikosi ili kiwe bora.
“Wapo wachezaji ambao wataongeza mkataba ndani ya timu, wengine wataondolewa kwa mkopo pia wapo ambao wataongezwa ndani ya timu.
“Tayari tumekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza ambaye yeye kila kitu kimekamilika kilichobaki kwa sasa ni mwalimu mwenyewe kuamua kumtumia akiona inafaa,” . Alisema Eng.Hersi ambaye ndie mkurugenzi wa uwekezaji kampuni ya Gsm inayoifadhili na kuidhamini klabu ya Yanga sc.