Site icon Sports Leo

Nizar Aahidi Makubwa Yanga sc

Kocha Msaidizi mpya wa Yanga, Nizar Khalifan amesema amejiunga na timu hiyo kushirikiana na benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kuhakikisha miamba hiyo inachukua taji la Ligi Kuu.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Nizar alisema atasaidiana kwa nguvu na akili yake yote na viongozi waliopo kutoa alichonacho kuendeleza dhamira ya klabu hiyo.

“Nimshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii, tulikuwa watano tulioomba lakini nimebahatika mimi, tutasaidiana kwa hali na mali kuendeleza dhamira ya Yanga,” alisema.

Nizar aliyekuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza ya African Lyon amewahi kuzichezea timu mbalimbali kama Singida United, Pamba, Moro United na Vancouver Whitecaps ya Canada.

Exit mobile version