Kufuatia kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa timu ya daraja la chini ya Watford katika mchezo wa ligi kuu soka nchini Uingereza mkufunzi wa Man Utd huenda akatimuliwa muda wowote kuanzia Jumapili hii.
Bodi ya klabu hiyo iliitisha mkutano wa dharura uliochukua masaa matano baada ya kipigo hicho kujadili hatima ya mshambuliaji huyo wa zamani wa timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford Manchester.
Sehemu kubwa ya wajumbe wa bodi na wafanyakazi wa klabu hiyo wanataka kocha huyo atimuliwe haraka iwezekanavyo,huku maamuzi ya mwisho yakiachwa kwa Joel Glazer mmiliki wa klabu hiyo na endapo ataidhinisha basi kibarua cha kocha huyo Mnorway kitakua kimefikia tamati.
Hata hivyo klabu hiyo inatafuta namna bora ya kuachana na kocha huyo kwa heshima kutokana na makubwa aliyofanya akiwa kama mchezaji wa timu hiyo,makubaliano ya kusitisha mkataba kwa pande zote mbili ndio kitu kilichopo mezani.
Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Ole kutokana na kuendwa zaidi na nyota wa timu hiyo Cristiano Ronaldo,makocha wengine wanaohusishwa ni Brendan Rodgers,Eric Ten Haag na Ralf Rangnick.