Home Soka Phoden Bora Epl

Phoden Bora Epl

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Manchester City Phil Phoden ameibuka kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa mwaka 2023/2024 baada ya kutangazwa kuchukua tuzo hiyo siku ya Jumamosi Mei 18 mwaka huu.

Katika Tuzo hizo  Foden huo amempiku mchezaji mwenzake, Erling Haaland, Declan Rice na Martin Odegaard wote wa Arsenal, Cole Palmer (Chelsea), Alexander Isak (Newcastle United), Ollie Watkins (Aston Villa), na beki wa Liverpool, Virgil van Dijk.

Kinda huyo mwenye miaka 23 msimu amecheza jumla ya michezo 34 ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza akifunga mabao 17 na kutoa usaidizi wa mabao 8 ambapo huku akifunga mabao matatu katika mchezo mmoja mara  mbili na kuifanya tuzo hiyo kama miliki halali ya klabu ya Man city kwani ni msimu wa tano mfululizo tuzo hiyo inaenda klabuni hapo.

banner

Manchester City tayari imetwaa taji la nne mfululizo baada ya kuifunga Westham United kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika siku ya jumapili Mei 19 na kufikisha alama 91 huku Arsenal akishika nafasi ya pili na alama 89.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited