Site icon Sports Leo

Polisi Warudi Kambini

Wachezaji wa timu ya Polisi Tanzania wamerejea kambini Moshi baada ya kumalizika kwa mapumziko waliyokuwa wamepewa na uongozi ya siku nane.

Mapumziko hayo yalitolewa kufatia timu ya Polisi Tanzania kutokuwa na mchezo wowote tangu pale timu hiyo ilipocheza mchezo wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Coast kwenye uwanja wa mkwakani Tanga mei 16 uliomalizika kwa Polisi Tanzania kuibuka na ushindi wa goli moja.

Baada ya kurejea kambini kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi, timu itanza mazoezi rasmi kesho kwenye viwanja vya TPC ili kujiwinda na mchezo unaofata wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaochezwa Juni 19 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

“Askari wa mwamvuli wamerejea wakiwa na Ari na morali ya kwenda kuhakikisha malengo ya timu kwa msimu huu yanaweza kufikiwa kwa kukusanya alama 12 kwenye michezo minne iliyosalia kuanzia ule wa Juni 19 dhidi ya Simba”.

Polisi Tanzania imesalia na michezo minne mitatu ikiwa mwenyeji dhidi ya Simba, Kagera na Mwadui na mchezo wa ugenini dhidi ya Ruvu ikiwa imejikusanyia alama 41 baada ya kucheza michezo 30.

“Umoja wetu ndio Nguvu yetu kuweza kutimiza malengo yetu”

Exit mobile version