Site icon Sports Leo

Rasmi Ettiene,Tff Wapeana Talaka

Shirikisho la mpira nchini (Tff) limeachana rasmi na kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Ettiene Ndayiragije baada ya kuamua kuvunja nae mkataba kwa makubaliano ya pande zote.

Awali taarifa zilizagaa kuhusu shirikisho hilo kuachana na kocha huyo huku ujio wa kocha Kim Poulsen ukichagiza tetesi hizo lakini taarifa rasmi iliyotolewa leo na shirikisho hilo imehitimisha suala hilo.

Ettiene ameingoza Stars katika michuano mbalimbali na kufanikiwa kuivusha mpaka katika michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) huku akitolewa katika hatua ya makundi.

Exit mobile version