Chama cha soka Afrika (CAF) kimetoa ratiba ya michezo ya awali ya mtoano kwa mashindano ya klabu bingwa na ile ya kombe la shirikisho kwa vilabu kufuzu makundi.
Ratiba hiyo inaonesha kuwa mechi za kwanza za raundi ya kwanza zinatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 10-12 septemba 2021 na marudiano kati ya tarehe 17-19 septemba 2021,mechi za kwanza za raundi ya pili ni kati ya tarehe 26-28 novemba na zile za marudiano ni kati ya tarehe3-5 mwezi disemba 2021.
Tanzania itawakilishwa na timu nne kwa msimu wa 2021/2022 ambazo ni Simba,Yanga kwa michuano ya klabu bingwa na Azam na Biashara kwa upande wa kombe la shirikisho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.