Site icon Sports Leo

Samatta atupia Europa league

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ameifungia timu yake mpya ya Royal Antwerp kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kombe la shirikisho la Ulaya maarufu kama Europa league.

Katika mchezo huo licha ya Samatta kufunga lakini timu yake ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki katika mchezo wa kwanza wa makundi wa kundi D.

Katika kundi hilo mshambuliaji huyo atakutana na waajiri wake waliomtoa kwa mkopo klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ambao walitoa sare y 1-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.

Matokeo mengine ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo.

1.Brondby 0-0 Sparta Prague

2.Rangers 0-2 Lyon

3.Monaco 0-0 Sturm Graz

4.PSV 2-2 Real Sociedad

5.Leicester 2-2 Napoli

6.Galatasaray 1-0 Lazio

7.Lokomotiv 1-1 Marseille

8.Midtyjlland 1-1 Ludogorets

9.Crvena Zveda 2-2 Braga

10.Leverkusen 2-2 Ferencvaros

11.Betis 4-3 Celtic

12.Dinamo Zagreb 0-2 West Ham

13.Rapid Wien 0-1 Genk

Exit mobile version