Site icon Sports Leo

Senzo CEO mpya Yanga SC

Klabu ya soka ya Yanga imemtangaza rasmi Bw Senzo Mbatha Masingiza kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kuteuliwa kwa Senzo katika nafasi hiyo mpya ndani ya Yanga kunatokana na utekelezwaji wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo na anakuwa ni mtu wa kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Senzo raia wa Afrika ya Kusini kabla ya kuwa kaimu mtendaji mkuu alikuwa akihudumu katika klabu hiyo kama mshauri hasa kuelekea katika mfumo wa mabadiliko,hivyo cheo chake hiko kipya sasa kitamfanya awe na nguvu ya kiutendaji katika kuhakikisha Yanga inapiga hatua kubwa katika kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya timu hiyo.

Mbatha aliwahi kuhudumu nafasi ya CEO katika klabu ya soka ya Simba kabla ya kuachana nayo na kutua kwa Wananchi ambako amepatiwa cheo hicho kikubwa.

Exit mobile version