Sports Leo

Simba mikononi mwa Wazambia,Biashara matumaini bado yapo

Klabu ya soka ya Simba imepangwa kucheza dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika hatua ya mwisho ya kombe la shirikisho Afrika kusaka tiketi ya kuingia makundi ya michuano hiyo.

Simba ilitolewa na Jwaneng Galaxy kwa goli la ugeni baada ya kuruhusu kichapo cha 3-1 nyumbani katika dimba la Mkapa kwenye hatua ya kwanza ya kombe la klabu bingwa kufuzu hatua ya makundi,hivyo kudondokea kombe la shirikisho.

Mchezo wa awali utachezwa Novemba 28 Jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana tarehe 5 Novemba nchini Zambia.

Katika hatua nyingine kumeibuka matumaini mapya kwa wawakilishi wengine kwenye michuano hiyo Biashara United walioshindwa kusafiri na kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly Tripoli,hii ni baada ya ratiba iliyotoka mchana huu kuonesha kuwa mshindi kati Al Ahly Tripol au Biashara United atacheza dhidi ya Stade Mallen ya Mali.

Hiyo ni faraja kwa Waatanzania ambao walisikitishwa baada ya timu hiyo kutoweza kwenda Libya licha ya kuwa na mtaji wa 2-0 ilioupata nyumbani.

Exit mobile version