Site icon Sports Leo

Simba Queens Mabingwa Wanawake

Timu ya wanawake ya Simba Queens wameibuka mabingwa wa ligi ya wanawake baada ya kuifunga timu ya Baobab Fc bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya wanawake nchini.

Timu hiyo inayonolewa na kocha Mussa Mgosi iliwapasa kusubiri mpaka dakika za mwishoni kupata bao kupitia kwa Aisha Jaffari na kufanikisha kufikisha alama 54 katika michezo yote huku wakipishana alama moja na Yanga Princess walioibuka na ushindi wa alama 53 baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 6-0

Exit mobile version