Site icon Sports Leo

Simba sc Baba Lao

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuifunga timu ya As Vita 1-0  katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika uliofanyika nchini Congo Drc.

Katika mchezo ambao ulitawaliwa na mbinu kutoka kwa makocha wa pande zote uliamliwa na bao la penati la dakika ya 60 iliyopatikana na ya beki wa As Vita kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na Chriss Mugalu kufunga penati hiyo kwa ustadi mkubwa.

Licha ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha Florent Ibenge ya kuwatoa mastaa kadhaa akiwemo Papy Tshitshimbi Simba sc ilifanikiwa kulilinda bao hilo mpaka dakika ya mwisho ya mchezo.

Simba sc inatarajiwa kutua nchini kesho jumapili na itakua na kibarua kingine cha kujiuliza mbele ya mabingwa wa Afrika Al- Ahly katika uwanja wa mkapa februari 23.

Exit mobile version