Site icon Sports Leo

Simba Sc ”Out”

Klabu ya Simba sc imetolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika licha ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs Fc ya nchini Afrika ya kusini.

Kipigo cha awali cha mabao 4-0 ilichokipata ugenini ndicho kimewaangusha kwani walitakiwa kushinda mabao 5-0 ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Mabao ya Simba sc katika mchezo huo yalifungwa na John Boko aliyefunga mawili dakika za 24 na 56 huku Cletous Chama akifunga la mwisho dakika ya 86 na mpaka mwamuzi kutoka Burundi akipuliza kipyenga mchezo ulibaki na mabao 3-o na Kaizer kufanikiwa kufuzu.

Exit mobile version