Home Soka Simba Sc Vs Al Ahly Robo Fainali Caf

Simba Sc Vs Al Ahly Robo Fainali Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc itakutana na klabu ya Al ahly Fc katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya droo ya kupanga timu hizo kufanyika leo jijini Cairo nchini Misri ambapo Simba sc itaanzia nyumbani kati ya Machi 29-31 huku marudiano yakifanyika nchini Misri baada ya siku saba.

Simba sc itakua na kibarua kigumu kufuzu mbele ya timu hiyo kutokana na namna inavyojua kucheza kwa hesabu kali katika hatua ya mtoano ikilinganishwa kuwa iliwatoa katika michuano ya AFL iliyofanyika iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana na Mamelod Sundowns kuibuka mabingwa.

Endapo itachanga karata vizuri klabu ya Simba sc walau inaweza kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na ukweli kuwa Al ahly ya sasa sio tishio sana kama ilivyokua zamani japo bado ni moja ya timu ngumu kufungika hasa katika michuano hiyo hatua za mtoano.

banner

Katika mchezo wa mwisho timu hizo zilipokutana zilitoka sare ya 2-2 hapa nchini kisha zikatoka sare ya 1-1 nchini Misri matokeo ambayo yaliwapa nafasi Al ahly ya kusonga mbele na walitolewa na Mamelod Sundowns katika hatua ya nusu fainali.

Kwa mujibu wa droo hiyo iliyofanyika jioni ya leo timu zote nane kila mmoja kapata wa kukutana nae huku ratiba kamili ikiwa kama ifuatavyo.

ROBO FAINALI
Simba SC vs Al Ahly
TP Mazembe vs Petro Atletico
Esperance vs ASEC Mimosas
Yanga SC vs Mamelodi Sundowns

NUSU FAINALI
Esperance/ASEC vs Yanga/Mamelodi Sundowns
TP Mazembe/Petro Atletico vs Simba/Al Ahly

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited