Sports Leo

Simba sc Yaahirisha Uzinduzi wa Jezi

Klabu ya Simba sc imeahirisha tukio la uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2021/2022 lililokua limepangwa kufanyika leo Septemba 4 jijini Dar es salaam huku matukio yote yakiwekwa pamoja katika maadhimisho ya wiki ya Simba sc kuanzia Septemba 13.

Awali klabu hiyo ilipanga kuzindua rasmi jezi hizo lakini jana ilitangaza kuanza kuziuza rasmi madukani baada ya jezi hizo kuvuja na kufanya mashabiki kuongeza presha kwa msambazaji aliyeamua kuuza kabla ya uzinduzi rasmi wa jezi hizo mapema hii leo.

Klabu hiyo imetoa Tangazo rasmi la kuahirisha uzinduzi huo masaa machache yaliyopita kupitia mitanda yake ya kijamii japo maamuzi hayo yalitegemewa na mashabiki wengi kutokana na hali halisi iliyojitokeza.

Exit mobile version