Site icon Sports Leo

Simba sc Yafuzu Kibabe

Klabu ya Simba sc imefuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuitandika Fc Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Platnum waliingia wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa awali walijikuta wakifanya faulo nyingi na kusababisha Simba sc kupata penati dakika ya iliyofungwa kiufundi na Erasto Nyoni dakika ya 38.

Dakika ya 61 kipindi cha pili shuti la Rally Bwallya lilipanguliwa na kipa wa Fc Platnum na kumkuta Shomari Kapombe aliyefunga bao la pili huku John Bocco na Cletous Chama wakifunga bao la tatu na nne dakika za 90 na 95.

Simba sc inaingia katika hatua ya makundi ya klabu bingwa ikiwa na mara ya pili kwa miaka ya hivi karibuni baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018/2019 ambapo ilitolewa hatua ya robo fainali na Tp Mazembe.

Exit mobile version