Simba Sc Yaipiga Jkt Tanzania 2-1

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba SC imeendelea kuonesha ubora na nia ya kurudisha taji la Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji JKT Tanzania, katika mchezo mkali uliopigwa Novemba 9, 2025 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliovuta hisia za watazamaji, Simba ililazimika kufanya kazi ya ziada baada ya JKT Tanzania chini ya kocha Ahmed Ally kuanza kwa kuwadhibiti vizuri wapinzani wao na kulinyima muda mrefu lango lao fursa za wazi za Simba sc kupata mabao kipindi cha kwanza, hali iliyowafanya mashabiki kuanza kuingiwa na wasiwasi kwa dakika 45 za mwanzo.

Kipindi cha kwanza kilimalizika bila kufungana, licha ya Simba kushambulia kwa vipindi kadhaa kupitia washambuliaji wao hatari Neo Maema na Steven Desse Mukwala ambao mara kadhaa walilazimishwa kupiga mashuti ya mbali kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya Jkt.

JKT Tanzania walionekana kuingia katika kipindi cha pili wakiwa na morali ya juu na mipango mipya ya kiufundi, na haikuchukua muda kuonyesha dhamira yao. Dakika za mwanzo za kipindi cha pili, nahodha wao jasiri Edward Songo aliwakosesha usingizi mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao la kuongoza akiunganisha pasi safi iliyowekwa kwenye eneo hatari na mshambuliaji Paul Peter Kisunda na kumwacha kipa wa Simba Yakoub Suleiman bila la kufanya.

banner

Bao hilo liliamsha presha kwa kocha Goran Pandev akalazimika kuongeza kasi ya mashambulizi huku kiungo mshambuliaji Ellie Mpanzu akianza kutawala eneo la kati kwa ustadi mkubwa. Hatimaye juhudi hizo zikazaa matunda dakika ya 63 baada ya Mpanzu kutengeneza krosi tamu iliyomkuta Wilson Nangu ndani ya eneo la hatari. Bila kigugumizi, staa huyo akapiga kichwa maridadi kilichompoteza kipa wa JKT na kuiweka Simba kwenye mizani sawa 1-1.

Simba Sc Yaipiga Jkt Tanzania 2-1-www.sportsleo.co.tz

Bao hilo liliwaamsha kabisa wachezaji wa Simba ambao walianza kutandaza soka la kasi na pasi fupi fupi tamu, wakionekana kutaka ushindi kuliko kuridhika na pointi moja. Dakika ya 73, mashambulizi ya Simba yakazaa bao la pili kupitia kwa kinara wao wa ushambuliaji, Jonathan Sowah. Straika huyo alimalizia kazi nzuri ya Morice Abraham aliyedhibiti mpira kwa utulivu ndani ya boksi kabla ya kumsetia Sowah aliyefunga kwa ustadi mkubwa na kuwafanya mashabiki wa Simba kuruka juu kwa furaha.

Baada ya bao hilo, Simba waliendelea kutawala mchezo wakihakikisha hawarudi nyuma tena kwa kuruhusu madhara. JKT Tanzania licha ya kupambana hadi dakika ya mwisho, walishindwa kupata bao la kusawazisha mbele ya ulinzi imara wa mabingwa hao wa zamani wa Tanzania Bara.

Simba Sc Yaipiga Jkt Tanzania 2-1-www.sportsleo.cotz

Kabla ya kipenga cha mwisho, mashabiki wa JKT walionekana kushusha pumzi ndefu kutokana na kiwango kizuri walichoonyesha timu yao dhidi ya moja ya vigogo wa soka nchini. Hata hivyo, Simba waliendelea kuokuonyesha ubora katika kulinda matokeo mpaka dakika 90 zilipokamilika.

Kwa ushindi huo, Simba SC sasa inasalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 9 baada ya kushinda michezo yake yote mitatu ya mwanzo wa msimu, jambo linalotuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao wakubwa Yanga SC na Azam FC kwamba moto umeanza kuchoma mapema.

Mchezo huo umeacha taswira kwamba Simba imerejea katika hali yake ya kinyama msimu huu, ikionesha uwezo wa kupindua matokeo na kupambana hadi dakika ya mwisho. Kinachosubiriwa sasa ni kuona kama wataendelea na kasi hiyo kwenye michezo inayofua

You may also like

Leave a Comment

Enable Notifications OK No thanks