Mabosi wa klabu ya Simba sc wakiongozwa na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez wamekana kuhusu kuwa na mpango wa kumuajiri kocha Mwinyi Zahera kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo.
Awali taarifa zilisambaa ziidai kuwa mwenyekiti na mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji ana mpango wa kumuajiri kocha huyo ili kusaidiana na kocha mpya Didier Gomez kupeperusha bendera ya klabu hiyo kimataifa.
“Sio kweli hata kidogo. Kwanza hata simfahamu huyo Mwinyi Zahera, namsikia tu. Huyo mtu hayupo kwenye benchi letu la ufundi, leo tutaiweka sawa.”
“Kuna watu watatu wamejiunga na benchi letu la ufundi hivi karibuni, Kocha Mkuu, Kocha wa Magolikipa na mtu mwingine tunamtangaza leo.”Alisema Ceo Barbara wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds Fm.