Home Soka Simba Sc,Al Hilal Zamtaka Dube

Simba Sc,Al Hilal Zamtaka Dube

by Sports Leo
0 comments

Klabu za Simba sc na Al Hilal Fc ya Sudan zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji Prince Dube wa klabu ya Azam Fc baada ya kutuma ofa katika klabu hiyo ambayo siku za karibuni imeingia katika mgogoro wa kimkataba na mchezaji huyo.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam Fc imeonyesha kuwa klabu hiyo imepokea rasmi ofa kutoka vilabu hivyo vikiwa na nia ya kumsajili mfungaji huyo lakini mpaka sasa ofa hizi zinajadiliwa huku pia klabu hiyo imezialika klabu nyingine zenye nia ya kumsajili kuwasilisha ofa zao.

Mpaka sasa haijafahamika kama klabu ya Yanga sc nayo itawasilisha ofa kumtaka staa huyo ambaye inahusishwa nae kutaka kumsajili ama la huku nia ya mchezaji huyo ikiwa ni kuwa huru na sio kusajiliwa na klabu nyingine moja kwa moja.

banner

Dube ambaye ana mkataba wa miaka miwili na nusu kusalia Chamazi tayari ameondoka klabuni hapo baada ya kuwasilisha barua ya kuvunja mkataba akidai kutokua na furaha kuendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na kutokua na njaa ya mataji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited