Kupitia mtandao wa AS-Far.com, kocha wa zamani wa Simba SC Tanzania ambaye hivi sasa anaifundisha klabu ya FAR Rabat amesema licha ya klabu yake ya zamani kuwa na wachezaji wazuri na wenye ubora mkubwa lakini hafikiri kuwasajili kwasababu tayari wachezaji hao wana mikataba na Simba na ili kuwasaji unatakiwa ulipe kiasi cha pesa kisichopungua $1m (dola milioni moja).
“Licha ya Simba kuwa na wachezaji wazuri sana lakini sifikirii kusajili mchezaji yeyote kutoka katika klabu hiyo kwasababu tayari klabu ya Simba imewasainisha mikataba mirefu hivyo ili kuwapata itakubidi uwalipe ada ya usajili kiasi cha pesa kisichopungua dola milioni moja” alisema Sven
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.