Site icon Sports Leo

Solskajer bado amtamani Lingard Man Utd

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer bado anatamani kuendelea kupata huduma ya kiungo mshambuliaji Jesse Lingard katika klabu hiyo licha ya mchezaji huyo kutaka kuondoka katika viunga vya Old Trafford.

Lingard mkataba wake unatarajia kutamatika Julai mwakani huku akiwa huru kufanya mzaungumzo na klabu yoyote inayomhitaji mwezi Januari.

Mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya baina ya mashetani hao wekundu na Lingard yamevunjika baada ya mchezaji huyo kuhisi kusalitiwa na Ole kwa kutompa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.

Mchezaji huyo alifanya vizuri alipokuwa West Ham United kwa mkopo katika duru ya pili ya ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita ambapo alionyesha kiwango safi kwa kufunga jumla ya magoli 11 katika kipindi cha miezi minne tu.

Man Utd walikataa dau la paundi milioni 18 kutoka kwa wagonga nyundo hao wa London wakiamini angesaini mkataba mpya na kuuzwa kwa bei kubwa hali ambayo haionekani kutokea.

Katika mkutano na waandishi wa habari hii leo Ole amesema kuwa Lingard ni mchezaji muhimu mno katika klabu hiyo na anaamini bado wana nafasi ya kumshawishi kusalia katika timu hiyo licha ya kutaka kutolewa kwa mkpo mwezi Januai katika dirisha dogo.

Exit mobile version