Site icon Sports Leo

Spurs yamgeukia Nuno

Klabu ya Tottenham hotspurs ya Uingereza imeanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu ya Wolves Mreno Nuno Espirito Santo. Hatua hiyo imekuja baada ya klabu hiyo kushindwa katika majaribio kadhaa ya kuwanasa makocha wakubwa duniani ambao hawakuvutiwa na mipango ya klabu hiyo.

Nuno hakuwa kwenye orodha ya awali ya makocha wanaohitajika na  Tottenham hadi alipowasili mkuruenzi mpya wa klabu hiyo Fabio Parattici ambaye ndiye aliempendekeza kuwa kocha mpya wa klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Nuno aliachana na klabu ya Wolves baada ya kumaliza kwa msimu wa ligi ya Uingereza 2020/2021 baada ya kuhudumu katika timu hiyo kwa miaka zaidi ya minne.

Exit mobile version