Musa Kisoki ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha wacheza soka Tanzania (SPUTANZA) amefunguka na kuthibitisha kuwa mchezaji Asante Kwasi alikuwa mwanachama wao na kamwe afikirii kuwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA linaweza kuwafungia Simba bila kuwasiliana nao
“Kwasi alikuwa mwanachama na hakuwai kutamka kuwa anaidai klabu ya Simba na hilo nathibitisha na hatujawai kumshughulikia madai yake ya kuidai klabu ya Simba
“Pia ningetoa kutoa ufafanuzi Kwasi kwenda kwenye Chama cha Ghana kimshughulikie madai yake ambayo yapo nchini Tanzania inakuwa sio sahihi na hao FIFA kwa kanuni zao hawawezi wakaifungia moja kwa moja Simba kwa kuipa adhabu bila kuwapa taarifa na kuwauliza.
“Vitu hivi vipo kikanuni hawakurupuki lazima wangekuwa wameiandikia barua kama wanadaiwa na Kwasi ili wajieleze na watoe ufafanuzi kamili, kuwafungia moja kwa moja sio sahihi wala sio kweli.