Site icon Sports Leo

Stars,Libya Bila Mashabiki

Kuna uwezekano mkubwa wa Mashabiki kutopata fursa ya kuingia uwanjani kutazama mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) baina ya Taifa Stars na Libya utakaochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 29.

Hiyo inafuatia zuio la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa mechi hiyo na nyinginezo ikiwa ni hatua ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ingawa baadhi ya mechi zimepewa ruhusa ya kushuhudiwa na mashabiki viwanjani.

Mfano Nigeria yenyewe imeruhusiwa kuingiza 30% ya mashabiki katika mechi yake dhidi ya Lesotho,Stars inahitajika kushinda mchezo wa leo na mwingine zidi ya Libya siku ya Jumatatu ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu michuano hiyo.

Exit mobile version