Home Soka Sure Boy Ajifunga Miwili Yanga sc

Sure Boy Ajifunga Miwili Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Yanga sc imemuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wake Salum Abubakar “Sure Boy” kuendelea kukipiga kunako klabu hiyo baada ya ule wa awali kufika tamati katika usajili wa dirisha dogo.

Kiungo huyo alijiunga na Yanga sc iliyokua chini ya kocha Nasredine Nabi mnamo dirisha la januari msimu wa  2021/2024 ambapo baada ya miaka miwili ameamua kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili kusalia klabuni hapo ambapo kwa mujibu wa taarifa za ndani mkataba huo hauna maboresha ya mshahara.

Sure boy aliacha na Azam Fc baada ya kuitumia kwa takriban miaka 14 na kuamua kujiunga na Yanga sc ambao amekua na vipindi mbalimbali akipata nafasi chini ya Kocha Nabi huku msimu huu chini ya kocha Miguel Gamond amecheza jumla ya michezo sita katika mashindano yote.

banner

Msimu uliopita chini ya Nabi kiungo huyo alikua akipata nafasi mara kwa mara na alikua na mchango mkubwa katika kikosi hicho kiasi cha kufika fainali ya michuano ya kombe la shirikishho barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited