Site icon Sports Leo

Tarimba Alia na Michezo ya Kubahatisha

Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba ameishauri Serikali kuweka sharti la kila kampuni ya michezo ya kubahatisha [Betting] kudhamini timu ya michezo kama sharti la kupewa leseni ikiwa ni njia ya kurudisha kwa jamii.

Tarimba ambaye alikua meneja oparesheni wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportspesa ameahidi kulipeleka suala hilo Bungeni kama hoja binafsi ili liweze kufanyiwa kazi na mamlaka husika.

Endapo wazo hilo litafanyiwa kazi na kupitisha litasaidia kupunguza makali ya kuendesha klabu ambayo timu hukutana nazo kutokana na kuwa na uchache wa vyanzo vya mapato.

Exit mobile version