Site icon Sports Leo

Tizi La Mwambusi Usipime

Kocha Juma Mwambusi ameanza kutekeleza programu yake ya mazoezi leo kwa kuanza na dozi nene ya asubuhi na jioni kwa wachezaji wake.

Mara baada ya kukabidhiwa mikoba rasmi Kocha Mwambusi amewasilisha programu yake ambayo kwa siku Nne za mwanzo vijana watafanya mazoezi mara mbili kisha Ijumaa watafanya mara moja.

“Programu hii imelenga kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji lakini pia kujenga uwezo wa pamoja kama timu kutokana na mapungufu ambayo yalionekana kwenye kikosi,” amesema Kocha Mwambusi.

Amesema anaamini kikosi kitakaa sawa muda si mrefu na baada ya wiki hii ataangalia ratiba kama itaruhusu mchezo wa ndani wa kujipima mguvu.

Exit mobile version