Home Soka Tuzo Ligi Kuu Kutolewa Julai

Tuzo Ligi Kuu Kutolewa Julai

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limesema kuwa tuzo za wachezaji na makocha waliofanya vizuri msimu huu wa ligi kuu zitatolewa mwezi Julai wakati wa michuano ya Ngao ya jamii ambayo inaashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini.

Kawaida tuzo hizo hutolewa mapema baada ya ligi kumalizika ambapo mastaa mbalimbali huhudhuria tuzo hizo zikiwa bado na mvuto zaidi kama ilivyokua mwaka jana ambapo zilitolewa jijini Tanga siku masaa machache baada ya mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho baina ya Yanga sc na Azam Fc.

banner

Barua iliyotolewa na TFF imetaja kuwa sababu kubwa ya tuzo hizo kufanyika kipindi tajwa ni kuhakikisha zinakua na ubora wa hali ya juu sababu ambayo imeleta ukakasi miongoni mwa wadau wengi wa soka hapa nchini ambapo wamedai kuwa baadhi ya mastaa watakosa kushiriki tuzo hizo kutokana na ukweli kwamba mikataba yao ya soka na timu zao iko mwishoni.

Mastaa Stephen Aziz Ki na Feisal Salum wanatajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huku Loy Matampi wa Coastal Union akitarajiwa kuchukua tuzo ya kipa bora dhidi ya Djigui Diarra huku Aziz Ki akiwa tayari na uhakika wa kuchukua kiatu cha tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu ya Nbc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited