Kocha wa zamani wa klabu ya Simba sc Patrick Aussems ametimuliwa na klabu ya Black Leopard Fc ya nchini Afrika ya Kusini aliyojiunga nayo mwezi oktoba mwaka huu.
Kocha huyo ametimuliwa baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo alizokua benchi huku pia ikidaiwa alikua hana maelewano na uongozi wa klabu hiyo.
Kocha huyo alikua anahitaji kuishi hotelini lakini klabu hiyo ilimpa nyumba na gari badala ya matakwa yake ya awali ya kuishi hotelini suala ambalo uchebe hakupenda na inadaiwa alishamwambia wakala wake atafute timu licha ya kuwa na mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.