Mshambuliaji Thomas Ulimwengu Januari 6 aliisaidia TP Mazembe ya Congo kushinda mabao 2-1 dhidi ya Bouenguidi ambapo alikuwa miongoni mwa washambuliaji waliopeleka kilio kwa wapinzani hao mapema.
Ushindi huo uliopata klabu hiyo unamaanisha kwamba imefuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika ambapo dakika ya 14 alipachika bao la kuongoza ambalo liliwapa nguvu Mazembe na baadae walipachika bao la pili dakika ya 45 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 wakiwa Uwanja wa Stade TP Mazembe.
Mpaka mpira unaisha Bouenguidi walikubali kipigo hicho huku wakipata bao la kufutia machozi dakika ya 79 kupitia kwa Djoe Dayan Boussougou ila halikuweza kuwapa faida wapinzani hao kusong mbele hivyo watashiriki Kombe la Shirikisho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.