Site icon Sports Leo

Uwanja wa A/Mwinyi wawekewa nyasi bandia

Uwanja wa michezo wa Ali Hassani Mwinyi wa Mkoani Tabora umewekewa nyasi za bandia tayari kwa kutumika kwa mechi mbalimbali za kimashindano kama ligi daraja la kwanza,ligi kuu na kombe la shirikisho.

Hayo yamesema na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Hasani Kapela hii leo alipokuwa akifanya mahojiano na clouds tv katika kipindi cha 360.

Kapela amesema kuwa baada ya maagizo ya Rais Samia kutaka kuboreshwa kwa viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na CCM,wao kama Mkoa wamechukua maamuzi ya kutekeleza.

Aliendelea kusema kuwa wamefanya hivyo kwa kuwa suala la michezo ni kipaumbele kikubwa kwa Mkoa huku wakijipanga kupandisha timu kucheza ligi kuu ya soka ya NBC kutokana na hadhi ya uwanaj huo.

Tabora kwasasa ina wakilishwa na timi ya Kitayosce katika ligi daraja la kwanza ambapo inafanya vizuri hali inayowapa matumaini ya kucheza ligi kuu mwakani.Timu hiyo ina mastaa kadhaa kama nyota wa zamani wa Yanga Papy Tshishimbi na winga wa zamani wa Simba na TP Mazembe Deo Kanda.

Exit mobile version