Site icon Sports Leo

Wabunge Waishukia Tff,Basata

Baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania wametoa malalamiko kuhusu utendaji wa taaasisi za michezo nchini za shirikisho la soka(TFF) na baraza la sanaa la Taifa(Basata).

Wabunge hao wamesema hayo bungeni wakati wakichangia bajeti ya Wizara ya michezo sanaa na utamaduni ambapo mbunge Festo Sanga alilalamikia kuhusu utendaji wa vyombo hivyo nchini huku akiungwa mkono na mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma pamoja na Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi ambaye alilalamika suala la Tff kugeuka kuwa chombo cha kufungia fungia.

Exit mobile version