Site icon Sports Leo

Wamechapwa Tena

Kocha Jurgen Klopp ana maswali magumu ya kujibu hivi sasa baada ya kuwa na vipigo mfululizo katika klabu yake ya Liverpool kufuatia kukubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Manchester City.

Mabao ya Gundogan dakika ya 49 lililosawazishwa na Mo Salah dakika ya 63 huku akiongeza bao la pili kwa City dakika ya 73 na Rahim Sterling akifunga dakika ya 76 na bao la nne la City lilifungwa na Phil Phoden Dakika ya 83 na kupeleka kilio kwa mashabiki wa Liverpool katika uwanja wa nyumbani.

Kutokana na ushindi huo Man City wanashinda game yao ya Premier League kunako dimba la Anfield kwa mara ya kwanza tangu 2003.

Exit mobile version