Klabu ya Yanga imeendelea kuonesha makucha yake baada ya kumalizana na kiungo Patrick Sibomana kutoka Rwanda.
Yanga imezidi kuboresha kikosi chake kutokana na wachezaji wengi kumaliza mikataba yao msimu huu uliomalizika.
Sibomana anakuwa mchezaji wa tatu kumwaga wino Yanga baada ya Papy Tshishimbi na Issa Bigrimana kumalizana na timu hiyo.
Usajili huu umekuwa pendekezo la Kocha Mwinyi Zahera ambaye amekabidhiwa majukumu ya kuhakikisha anapendekeza wachezaji wanaopaswa kusajiliwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.