Site icon Sports Leo

Yanga Sc yabanwa mbavu Kagame

Klabu ya soka ya Yanga imeshindwa kutamba katika mchezo wa pili mfululizo kwenye michuano ya kombe la Kagame linalofanyika nchini Tanzania kwa msimu huu.

Mchezo huo uliofanyika katika dimba la Benjamin Mkapa Yanga imetoka suluhu na klabu ya Atlabara ya Sudan licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kutosha.

Yanga iliwachezesha nyota wake wapya Jimmy Ukonde pamoja na Diskson Ambundo lakini hawakuweza kuisaidia timu hiyo,na sasa watalazimika kushinda mchezo wao wa mwisho wa kundi lao dhidi ya vinara Express ya Uganda  ili kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Exit mobile version