Home Soka Yanga Sc Yachukua Alama 3 Mbeya

Yanga Sc Yachukua Alama 3 Mbeya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu muhimu mbele ya Tanzania Prisons baada ya kuifunga 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa  Sokoine mkoani Mbeya huku mashabiki lukuki wakifurika uwanjani hapo.

Iliwachukua Yanga sc dakika nane kupata bao la kwanza likifungwa na Clement Mzize aliyepokea pasi nzuri kutoka upande wa kulia mwa uwanja iliyopigwa na Pacome Zouzou na kuwaacha mabeki wa Prisons wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kushuhudia shangwe za mashabiki wa Yanga sc.

Yanga sc waliumiliki mchezo huku wakikosa mabao kadhaa ambapo Pacome Zouzou alifunga bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko na kuwaweka mbele Yanga sc mpaka mapumziko lakini kipindi cha pili makosa ya Bakari Mwamnyeto yalisababisha kipa Metacha Mnata kupata kadi nyekundi huku Prisons wakinufaika na faulo iliyopigwa na Jeremiah Juma dakika ya 64 ambapo aliiandikia bao Prisons.

banner

Baada ya bao hilo mchezo ulibadilika na kuwalazimu Yanga sc kupambana kupata alama tatu kutokana na kuwa pungufu lakini kadi nyekundu upande wa Prisons iliwarudisha mchezoni baada ya mwamuzi Ahmed Arajiga kumpa kadi nyekundu winga wa Prisons.

Mpaka dakika tisini zinatamatika Yanga sc ilichukua alama tatu na kufikisha alama 40 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa imecheza jumla ya michezo 15 ya ligi kuu nchini na tayari imekamilisha duru la kwanza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited