Site icon Sports Leo

Yanga sc Yamrejesha Kocha wa Shikhalo

Klabu ya Yanga imetangaza kumrejesha kikosini aliyewahi kuwa kocha wa makipa wa klabu hiyo Razak Siwa ambaye  raia wa Kenya ns anachukua nafasi iliyoavchwa na Vladimir Niyankuru aliyefutwa kazi hivi karibuni sambamba na aliyekuwa kocha mkuu Cedric Kaze.
Yanga pamoja na Siwa hawajaweka wazi mkataba ulioingiwa ni wa muda gani lakini kocha huyo amewahi kufanya kazi na Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikalo wakati wakiwa katika timu ya Bandari Fc ya nchini Kenya ambako Farouk aling’ara kiasi cha kutwaa tuzo ya kipa bora wa msimu nchini humo.
Huu ni muendelezo wa klabu ya Yanga kuliimarisha benchi lake la ufundi ambapo kwa sasa timu imekabidhiwa kwa Juma Mwambusi Hadi mwishoni mwa msimu huu.

Exit mobile version