Site icon Sports Leo

Yanga sc Yatangaza Mkutano Mkuu

Klabu ya Yanga sc imetangaza tarehe 27 mwezi wa sita kuwa itafanya mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo baada ya kutofanyika takribani miaka mitatu.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya habari ya klabu hiyo imesema kwamba mkutano huo mkuu utafanyika tarehe tajwa huku ikiwaomba wanachama wa klabu hiyo kulipia mapema kadi zao za uanachama ili wapate nafasi ya kuhudhuria mkutano huo mkubwa.

Wadau wengi wa soka nchini hasa wanachama wa kklabu hiyo wanategemea mkutano huo utapitisha ajenda ya mabadiliko ambapo klabu hiyo itabadili umiliki kutoka ule wa wananchama na kwenda kwenye uwekezaji ambapo kutakua na muwekezaji atakayemiliki asilimia kadhaa.

Exit mobile version