Site icon Sports Leo

Yanga Sc Yatua Mapinduzi

Kikosi cha wachezaji 20 wa klabu ya Yanga sc kimetua salama visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la mapinduzi litakaloanza kesho mpaka tarehe 12 januari visiwani humo.

Kikosi cha Yanga sc kimetua visiwani humo kikiwa na mastaa kadhaa huku kikiwakosa baadhi ya nyota walioitwa timu za Taifa na wengine wamekua na majeraha na matatizo ya kifamilia huku Carlos Carinhos akiwa ni miongoni mwa mastaa walisafiri na timu hiyo.

Yanga sc itashuka dimbani kesho kuvaana na Jamhuri Fc ya mjini Pemba ambapo mechi hiyo itakua na mechi ya pili itakayochezwa jioni.

Exit mobile version