Uongozi wa Yanga umeweka wazi kwamba bado una imani na Kocha Mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze licha ya timu kushindwa kupata matokeo chanya ndani ya uwanja kwenye mechi za hivi karibuni.
Yanga mzunguko wa pili imeanza kwa kusuasua huku ikipewa presha kubwa kutoka kwa watani wao jadi Simba ambao kasi yao inazidi kuwa kubwa kila waingiapo ndani ya uwanja.
“Tunaimani na Kaze na matokeo ambayo tunayapata tunaamini kwamba ni sehemu ya mchezo kwa kuwa ikiwa tutashinda iwe ni kwa mabao mengi ama moja kinachotazamwa ni ushindi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Mashabiki wasiwe na presha imani yetu ni kwamba kila kitu kitakuwa sawa na mambo yatakwenda kwenye utaratibu ambao tunahitaji hakuna haja ya kuwa na presha”