Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga sc David Mwakalebela amesema kwamba tayari timu hiyo imeshalipa ada ya kusikiliza kesi ya Morrison katika mahakama ya kimataifa ya michezo duniani Cas.
Mwakalebela alisema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari akiwa Visiwani Zanzibar wakati timu hiyo ilipotwaa ubingwa wa kombe la mapinduzi.
“Jana ilikuwa ni deadline ya malipo, sisi kama klabu ya Yanga tulisema tumedhamilia kupata haki na malipo tulishafanya kwa hiyo tunasubiria kupangiwa kesi itafanyika lini”Alisema mwakalebela