Site icon Sports Leo

Yanga Yatoa Dozi Nene

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza ameng’ara katika mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya Yanga sc baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Singida United.

Saido licha ya kufunga mabao hayo dakika za 22 na 70 alionyesha kiwango kikubwa akitoa pasi nzuri za kufunga ambapo Waziri Junior na Ditram Nchimbi walikosa umakini kuzitumia.

Dakika ya 81 aliingia Deus Kaseke kuchukua nafasi ya Saido na kuipatia Yanga sc bao la tatu dakika moja baadae na kumaliza mechi kwa ushindi mnono wa pili mfululizo.

Exit mobile version