Sports Leo

Zahera,Kaze warejea Yanga

Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umeamua kuliongezea nguvu benchi la ufundi kwa kumuajiri kocha wao wa zamani Cedric Kaze kuwa kocha msaidizi wa Nasreedin Nabi pamoja na Mwinyi Zahera kuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya soka la vijana.

Mwinyi Zahera aliwahi kuifundisha Yanga msimu wa 2018/2019 na kumaliza nafasi ya pili katika msimu mgumu uliojaa ukata wa timu hiyo hadi kufikia kuchangisha michango kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo kila walipokuwa wakicheza ili kuwapa hamasha wachezaji kuipigania klabu hiyo,ametambulishwa hii leo na Mtendaji Mkuu wa mpito wa Yanga Senzo Mazingiza.

Mkongomani huyo ni kipenzi kiubwa cha Wananchi kwani aliivumilia sana timu hiyo katika kipindi kigumu bila kuiacha ikiwa na kutoa pesa yake binafsi ilipohitajika.

Kwa upande wa Kaze aliyetambulishwa kama msaidizi wa Nabi ataenda ataenda kuongeza nguvu benchi la Yanga kitaaluma baada ya Nabi kuanza bila msaidizi baada ya kuondoka kwa msaidizi aliyekuja naye mara ya kwanza.

Kaze ana kazi ya kuhakikisha klabu hiyo inatwaa mataji msimu baada ya kushindwa msimu uliopita alipokuwa kocha mkuu,hivyo hii ni nafasin nyingine kwake.

Exit mobile version