Home Soka Azam Fc ChupuChupu Kwa Walibya

Azam Fc ChupuChupu Kwa Walibya

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imeshindwa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya kombe la shirikisho nchini licha ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Akhdar Fc  uliofanyika nchini Jumapili usiku katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Ikiwavuta umati wa mashabiki baada ya kutokeweka kiingilia kabisa huku mashabiki wakipaswa kuvaa jezi za klabu hiyo kupata nafasi ya kuingia uwanjani klabu hiyo ilipata bao la kwanza kupitia kwa Idriss Mbombo na kuwachanganya waarabu hao ambapo kutokuwa na umakini kwa wasambuliaji wa Azam Fc ambao walikosa nafasi kadhaa za wazi ziliufanya mchezo kwenda mapumziko ikiongoza 1-0.

Ikifahamu inapaswa kushinda kuanzia mabao 3-0 na kuendelea klabu hiyo ilirudi kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao baada ya mchezaji wa Akhdar Fc Ededen Essien kujifunga dakika ya 59 ya mchezo huo uliokua na kasi kubwa.

banner

Al Akhdar walirudi nyuma na kuzuia sehemu kubwa ya kipindi cha pili ambapo walifanikiwa mpaka dakika ya 90 ya mchezo Azam Fc hawakuongeza bao na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-2 na wageni hao kujihakikishia kucheza play off ili kufuzu kwenda hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited