Haipoi Haiboi ndiyo msemo wanaousema mashabiki wa Azam fc baada ya klabu hiyo kuendelea kushusha vyma vya nguvu ka ajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini ambapo wamefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji Cheikh Tidiane Sidibe akitokea Teungueth inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Senegal.
Beki huyo wa kushoto amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo akiungana na kocha wake wa zamani wa klabu yake ya Teungueth Yousuph Dabo ambaye ametua Azam Fc tangu msimu uliopita lakini msimu huu ndio wa kwanza kwake kama kocha wa klabu hiyo.
Azam Fc baada ya kumtambulisha staa huyo ndio imemaliza usajili wake kama ilivyotangaza kuwa itasajili mastaa wanne pekee katika dirisha hili ambapo mmoja ni mzawa Feisal Salum huku beki huyo anaungana na Gibril Sillah na Alasane Diao kukamilisha usajili klabuni hapo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.