Home Soka Griezman Sasa Rasmi Barcelona

Griezman Sasa Rasmi Barcelona

by Sports Leo
0 comments

Imebainika kwamba mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann atajiunga na Barcelona msimu ujao baada ya kuitumika klabu hiyo ya jijini Madrid kwa miaka mitano kwa mafanikio makubwa.

Hayo yamethibitishwa na mtendaji mkuu wa Klabu ya Atletico Madrid Angel Gill Marin wakati akiongea na moja ya chombo cha habari ambapo alisema ilishajulikana toka machi mwaka huu kuwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 atajiunga na wana catalunya.

Taarifa hizo zinamaliza tetesi za muda mrefu za Barcelona kumhitaji mshambuliaji huyo huku pia akihusishwa na klabu za Manchester united na Paris st.German ya ufaransa

banner

Wiki iliyopita akiwa Ufaransa mchezaji huyo alinukuliwa akisema kuwa uvumilivu unahitaji kwa muda si mrefu itajulikana anaelekea wapi.

Griezmann aliongoza Ufaransa kutwaa ubingwa wa kombe dunia mwaka jana na amefanikiwa kufunga magoli 29 katika mechi 70 za timu ya taifa Ufaransa huku akiifungia klabu yake magoli  21 katika mechi 48 msimu huu

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited