Home Soka Prisons Fc Yaachana na Minziro

Prisons Fc Yaachana na Minziro

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya Tanzania Prisons Fc imeachana na kocha Fred Felix Minziro kwa makubaliano ya pande mbili baada ya uongozi wa timu hiyo kutoridhishwa na matokeo ya klabu hiyo katika michuano ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Minziro alijiunga na Prisons kama kocha mkuu akisaini mkataba wa mwaka mmoja kuanzia Julai 17 2023 ambapo sasa klabu hiyo baada ya mizunguko tisa ya ligi kuu ya Nbc imeamua kuachana na kocha huyo kutokana na matokeo mabaya ambapo mpaka sasa ipo katika nafasi ya 14 ikiwa na alama saba katika michezo tisa ya ligi kuu.

Sasa kikosi cha timu hiyo kitakua chini ya kocha msaidizi Shaban Mtupa ambaye atakua na kazi kubwa ya kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo ambayo imeruhusu jumla ya mabao 15 huku ikifungwa kila mchezo kasoro ule dhidi ya Singida Fountaine Gate Fc.

banner

Kuachana na kocha huyo mkongwe nchini kunaifanya Tanzania Prisons kuwa timu ya saba sasa kuachana na makocha wake wakuu ambapo inaungana na timu za Simba sc,Singida Fountain Gate Fc,Namungo Fc,Ihefu Fc,Mtibwa Sugar na Coastal Union Fc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited